1.KUTOJUA GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA UNAYOTAKA KUJENGA
watu wengi hujikuta wanatumia gharama za ujenzi kubwa tofauti na walivo tegemea katika ujenzi wa nyumba zao .. Unapotaka kujenga nyumba Yako kabla haujaanza kujenga nyumba jua roughly budget ya makadirio ya gharama za ujenzi ya nyumba Yako.
Ramani Nyumba inaweza kuwa ni Ile Ile aliyojenga Mr John lakini gharama za ujenzi wa hiyo nyumba wewe na Mr John zisifanane hata kidogo kutokana na sababu mbali MBALI MBALI
Unapo kuwa unajua gharama za ujenzi roughly unazoweza kutumia itakuasaidia kufocus , kuondoa majuto na kujihakikishia kuwa nyumba itajemgwa na kuangalia ni namna gani utaweza kupata hiyo fedha Kwa ajili ya ujenzi.
Mfano umeongea na fundi tu mtaani, ukamuuliza hii nyumba unagharimi shingapi, akakwambia million 20 tu … mnaanza kujenga unajikuta mmeishia tu kwenye msingi unaanza kujuta na kujiambia Bora usingeanza
Wakati wa kutathimi gharama za ujenzi tumia Watalamu
2.KUTO KUFANYA MAANDALIZI YA KUTOSHA NA YA KINIFU WA NYUMBA UNAYOTAKA KUJENGA KABLA HAUJAANZA KUFANYA UJENZI
Katika safari ya ujenzi wa nyumba Yako mhusika mkuu ni wewe Kila hatua unatakiwa uwajibike kuanzia kwenye kuaandaa eneo la ujenzi mpaka kuingia katika hiyo nyumba
Kabla haujaanza kujenga nyumba Yako,Jiulize haya Maswali yatakusaidia
Ni aina gani ya nyumba nataka kujenga , ni ni Kwa Nini nataka kujenga aina hii ya nyumba ?
Nitajenga nyumba yenye ukubwa gani ? hapa ukizingatia kuhusu familia Yako kama ni kubwa au mdogo, au ni familia inayokua
Nitapata wapi pesa za ujenzi na je inaweza kigharimu shingapi?
Nijenge Kwa mara Moja au Nijenge Kwa awamu ?
Au kutoka na mahitaji yangu siwezi kupata nyumba kama hiyo na nikanunua kuliko nikasubiri mpaka mchakato wote wa ujenzi
Watalamu wapi watanisaidia katika ujenzi wa nyumba yangu ?
Ni design gani ya nyumba itanifaa zaidi ?
Ni Mimi tu wa kufanya maamuzi ya ujenzi ya nyumba au mke wangu watoto natakiwa kiwashirikisha ?
3.PANGA MIPANGO YAKO KABLA HAUJAANZA UJENZI WA NYUMBA YAKO ( PLAN BEFORE START BUILDING)
Jiandae kabla haujaanza ujenzi,usipo fanya hivo utaishia
kuwa na madeni yasiyo kuwa na ulazima ( au kuwa na deni kubwa kuliko hata uwezo wako wa kifedha)
kujutia maamuzi uliyofanya katika ujenzi wa nyumba Yako
kujutia design ya nyumba uliyojenga
4.KUTOKUWA NA MAONO YA NYUMBA UNAYOTAKA KUJENGA*
Nyumba Yako kabla haujaiona Kwa macho ya nyama uwe umesha ingia katika hiyo nyumba
Katika ujenzi wa nyumba Kila kitu ni Cha muhimu sana ndivyo vinatakavyo fanya. uifurahie nyumba Yako fikiria sebule Yako unataka iwaje , master bedroom ,jiko. , muonekano muingiliano wa NYUMBA na Kila kitu Cha muhimu katika nyumba ( you need to have a full picture of your homes in your head )
5.KUTOKUWA NA UELEWA JUU YA UKUBWA WA VIWANJA NA NYUMBA UNAYOTAKA KUJENGA
Tumeona wengi hapa wakipata changamoto , kweli kuwa na kiwanja ambacho hakikidhi aina au ukubwa wa nyumba anayotaka kujenga .. kiwanja kuwa kidogo sana ukilinganisha na nyumba anayotaka kujenga hapo
BLCHOMES tunauza viwanja piah kabla hatujaamuuzia mteja kiwanja huwa tuna muuliza mteja Maswali ili Kwa pamoja aweze kufanya maamuzi sahihi sio tu amenunua kiwanja
Kabla haujanunua kiwanja jiulize
jua katika hicho kiwanja unataka kujenga Nini ?
UKUBWA wa kiwanja utakindi mahitaji Yako ya jengo au nyumba unayotaka kujenga
kiwanja hakina changamoto yoyote ki jografia ? n.k
6.KUTOTUMIA WATALAAMU WA UJENZI
Kila kitu kina taaluma yake. Tabia ya kujifanya ujajua Kila kitu hauhitaji msaada ni kitu kibaya sana hasa katika safari ya ujenzi wa nyumba Yako . katika ujenzi wa nyumba Yako Kun Watalamu mbali MBALI utakao watumia kukamilisha nyumba Yako …tumia Watalamu wa UJENZI kukamilisha ujenzi wa nyumba Yako ili kuepuka hasara kubwa unayoweza kupata kama wengine walivyoshuhudia na kuepuka kusema .. ninge ninge nyingi
YAPO MAKOSA MENGI HAYO NI BAADHI TU
kama upo humu ndani hatutamani na wewe uwe mmoja wapo ya kufanya kosa lolote katika safari Yako ya ujenzi wa nyumba Yako
kama unakosa ulishawah kufanya katika ujenzi share na sisi kwenye comment au inbox wengine wasifanye Hilo kosa
JENGA NYUMBA YAKO NA BLCHOMES
WASILIANA NASI ZAIDI KWA MAELEZO ZAIDI NA KUPATA USHAURI BURE
WASILIANA NASI KUWEKA APPOINTMENT
0742892195 CALL/ TEXT/WHATSAPP
BLCHOMES,FEEL@HOME