BLC HOMES

CONTACT US: 0742892195

KUNUNUA vs  KUJENGA NYUMBA,Kipi ni Bora zaidi?

Katika mchakato wa kumiliki nyumba yako unaweza kukumbana na maamuzi ya kufanya …   ili kufikia kumiliki nyumba ya ndoto yako

Una machaguo mawili  ya kufanya Kati ya KUNUNUA au Kujenga mwenyewe nyumba yako from scratch.

Kipi ni bora Kati ya KUNUNUA nyumba au Kujenga mwenyewe

kuamua kujenga au KUNUNUA  nyumba  Kuna faida na hasara hasara zake 

Naamini  kila mtu anapenda  nyumba nzuri iwe ya KUNUNUA au Kujenga mwenyewe

Na kila mtu huwa anakuwa na sababu zake za kuchagua KUNUNUA  au Kujenga  

kujua faida na hasara za kujenga nyumba kunaweza  kusaidia kufanya maamuzi sahihi  katika kufikia   lengo lako la kumiliki  nyumba

Tuangalie   baadhi ya faida na hasara za kujenga na kununua nyumba

   FAIDA  ZA KUJENGA NYUMBA

•Unapata nyumba kulingana na mahitaji yako

ukiamua kujenga nyumba yako mwenyewe utaweza kujenga nyumba kulingana na mahitaji yako mwenyewe   inayokidhi life stye  yako   kuanzia muundo wa nyumba yako na muonekano wa nje unaotaka iwe na finishing  .. tofauti na ukinunua nyumba   katika nyumba unayonunua  huwezi kupata kila kitu ambacho unataka kiwe kwenye nyumba yako.

• Upya wa nyumba

 Hakuna kitu kizuri  kupata kitu  kikiwa kipya na ukakizindua mwenyewe kutumia. ukijenga nyumba yako mwenyewe  utapata experience ya  kuanza kutumia nyumba yako mwenyewe ikiwa mpya  kabisa tofauti na ukinunua nyumba ambayo tayari ilikuwepo.

Pamoja na hizo faida Kuna hasara za kujenga nyumba

hizi ni baadhi

• Kujenga nyumba ni gharama  kuliko KUNUNUA.

Takwimu zinaonesha  kujenga nyumba inaweza kugharimu wastani  asilimia  20_30 %zaidi  ukilinganisha na kununua

ukianza kupiga  mahesabu utagundua  kujenga nyumba yako mwenyewe ni gharama  kuliko KUNUNUA. Ni gharama nyingi ambazo zitahitajika kuhakikisha unakamilisha ujenzi wa nyumba

• Kusubiria  .. 

kujenga nyumba yako Kuna hitaji vitu vingi Sana  mpaka  nyumba kukamilika  kwa hiyo  inachukua mda  . mda wa kusubiria itategemea na aina ya nyumba ya nyumba unayojenga na  Kasi ya wanaojenga nyumba yako  wakati wa kusubiria  unatakiwa uwe. tayari kulipia  Kodi ya sehemu unauoishi

•Kuna gharama zilizojificha .. (hidden costs)

Kuna gharama za ujenzi wa nyumba ambazo zimefichika  ukiwa unawaza kujenga nyumba yako huwezi kizifikiria moja kwa moja  lakini ukiwa katika mchakato wa ujenzi. ndio utaweza kuziona …  ndio Mana unapoamua kujenga nyumba yako ni vizuri kufanya kazi na wataalamu ili upate  muongozo  katika mchakato wa ujenzi wa nyumba yako   kwa sababu   kina vitu ambavuo huwezi kufanya mwenyewe

• Stress ,..

katika mchakato wa kujenga nyumba Kuna vitu vingi ambavyo unatakiwa kufanya  na vingi ambayo hauna utaalamu navyo ..utahitaji kupata eneo la kujenga  , kujua aina ya nyumba unayotaka kujenga  (design)  na kusimamia kila chochote kinachohusu ujenzi wa nyumba yako na vyote vifanyike   bila makosa  . huu mchakato wote sio rahisi

FAIDA ZA KUNUNUA NYUMBA

• Inaweza kuchukua mda mchache

 ukiamua KUNUNUA nyumba unaweza usitumie mda mwingi Sana kuipata nyumba kuliko ukiamua kujenga mwenyewe.

• Sio gharama

kununua nyumba inaweza isiwe gharama Sana tofauti na  kujenga ,unaweza kupata nyumba nzuri na sehemu nzuri kwa Bei nzuri yu lakini ukilinganisha katika Hilo eneo  kununua  Kiwanja na kufanya ujenzi inakuwa gharama Sana.

HASARA ZA KUNUNUA  NYUMBA

•Ni ngumu kupata nyumba yenye kila kitu  ambacho unakihitaji 

•Inaweza kuchukua mda mrefu  na juhudi nyingi. kupata nyumba

Hizi ni baadhi ya faida na hasara za kununua au Kujenga nyumba 

Kama ni Mara yako ya kwanza  kuwa na mchakato wa kujenga nyumba  or kumiliki nyumba inaweza kuwa ni ngumu kuchagua au kufanya maamuzi Kati ya KUNUNUA au Kujenga nyumba yako

kutokana  na maelezo haya ambayo umepata  unaweza kuamua kafanya maamuzi

kila mtu ana sababu zake za kuchagua kujenga au KUNUNUA nyumba

kujenga nyumba ni gharama kuliko KUNUNUA

Takwimu zinaonesha kujenga nyumba ni gharama    kwa. 20-30 %  zaidi kulilo kununua

USHAURI MUHIMU

Iwe unaamua kununua au Kujenga nyumba yako  hakikisha unajenga nyumba  au KUNUNUA nyumba ambayo unaweza kumudu gharama zake  na ni nyumba utakayoifurahia

Uwe unataka kujenga nyumba au kununua  blchomes  tutaweza kukusaidia  kufikia malenho Yako

Blchomes tutakusaidia  kujenga nyumba yako ya kisasa , kuchora ramani , kujua makadirio ya ujenzi (.  BOQ   ) na kufanya maboresho ya nyumba yako wasiliana nasi zaidi kupata ushauri bure , na NAMNA TUNAVYOWEZA  kukamilisha ujenzi wa nyumba  yako Wasiliana nasi zaidi whatsapp 0742892195

1 thought on “KUNUNUA vs  KUJENGA NYUMBA,Kipi ni Bora zaidi?”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *