Katika mchakato wa kumiliki nyumba yako unaweza kukumbana na maamuzi ya kufanya … ili kufikia kumiliki nyumba ya ndoto yako
Una machaguo mawili ya kufanya Kati ya KUNUNUA au Kujenga mwenyewe nyumba yako from scratch.
Kipi ni bora Kati ya KUNUNUA nyumba au Kujenga mwenyewe
kuamua kujenga au KUNUNUA nyumba Kuna faida na hasara hasara zake
Naamini kila mtu anapenda nyumba nzuri iwe ya KUNUNUA au Kujenga mwenyewe
Na kila mtu huwa anakuwa na sababu zake za kuchagua KUNUNUA au Kujenga
kujua faida na hasara za kujenga nyumba kunaweza kusaidia kufanya maamuzi sahihi katika kufikia lengo lako la kumiliki nyumba
Tuangalie baadhi ya faida na hasara za kujenga na kununua nyumba
FAIDA ZA KUJENGA NYUMBA
•Unapata nyumba kulingana na mahitaji yako
ukiamua kujenga nyumba yako mwenyewe utaweza kujenga nyumba kulingana na mahitaji yako mwenyewe inayokidhi life stye yako kuanzia muundo wa nyumba yako na muonekano wa nje unaotaka iwe na finishing .. tofauti na ukinunua nyumba katika nyumba unayonunua huwezi kupata kila kitu ambacho unataka kiwe kwenye nyumba yako.
• Upya wa nyumba
Hakuna kitu kizuri kupata kitu kikiwa kipya na ukakizindua mwenyewe kutumia. ukijenga nyumba yako mwenyewe utapata experience ya kuanza kutumia nyumba yako mwenyewe ikiwa mpya kabisa tofauti na ukinunua nyumba ambayo tayari ilikuwepo.
Pamoja na hizo faida Kuna hasara za kujenga nyumba
hizi ni baadhi
• Kujenga nyumba ni gharama kuliko KUNUNUA.
Takwimu zinaonesha kujenga nyumba inaweza kugharimu wastani asilimia 20_30 %zaidi ukilinganisha na kununua
ukianza kupiga mahesabu utagundua kujenga nyumba yako mwenyewe ni gharama kuliko KUNUNUA. Ni gharama nyingi ambazo zitahitajika kuhakikisha unakamilisha ujenzi wa nyumba
• Kusubiria ..
kujenga nyumba yako Kuna hitaji vitu vingi Sana mpaka nyumba kukamilika kwa hiyo inachukua mda . mda wa kusubiria itategemea na aina ya nyumba ya nyumba unayojenga na Kasi ya wanaojenga nyumba yako wakati wa kusubiria unatakiwa uwe. tayari kulipia Kodi ya sehemu unauoishi
•Kuna gharama zilizojificha .. (hidden costs)
Kuna gharama za ujenzi wa nyumba ambazo zimefichika ukiwa unawaza kujenga nyumba yako huwezi kizifikiria moja kwa moja lakini ukiwa katika mchakato wa ujenzi. ndio utaweza kuziona … ndio Mana unapoamua kujenga nyumba yako ni vizuri kufanya kazi na wataalamu ili upate muongozo katika mchakato wa ujenzi wa nyumba yako kwa sababu kina vitu ambavuo huwezi kufanya mwenyewe
• Stress ,..
katika mchakato wa kujenga nyumba Kuna vitu vingi ambavyo unatakiwa kufanya na vingi ambayo hauna utaalamu navyo ..utahitaji kupata eneo la kujenga , kujua aina ya nyumba unayotaka kujenga (design) na kusimamia kila chochote kinachohusu ujenzi wa nyumba yako na vyote vifanyike bila makosa . huu mchakato wote sio rahisi
FAIDA ZA KUNUNUA NYUMBA
• Inaweza kuchukua mda mchache
ukiamua KUNUNUA nyumba unaweza usitumie mda mwingi Sana kuipata nyumba kuliko ukiamua kujenga mwenyewe.
• Sio gharama
kununua nyumba inaweza isiwe gharama Sana tofauti na kujenga ,unaweza kupata nyumba nzuri na sehemu nzuri kwa Bei nzuri yu lakini ukilinganisha katika Hilo eneo kununua Kiwanja na kufanya ujenzi inakuwa gharama Sana.
HASARA ZA KUNUNUA NYUMBA
•Ni ngumu kupata nyumba yenye kila kitu ambacho unakihitaji
•Inaweza kuchukua mda mrefu na juhudi nyingi. kupata nyumba
Hizi ni baadhi ya faida na hasara za kununua au Kujenga nyumba
Kama ni Mara yako ya kwanza kuwa na mchakato wa kujenga nyumba or kumiliki nyumba inaweza kuwa ni ngumu kuchagua au kufanya maamuzi Kati ya KUNUNUA au Kujenga nyumba yako
kutokana na maelezo haya ambayo umepata unaweza kuamua kafanya maamuzi
kila mtu ana sababu zake za kuchagua kujenga au KUNUNUA nyumba
kujenga nyumba ni gharama kuliko KUNUNUA
Takwimu zinaonesha kujenga nyumba ni gharama kwa. 20-30 % zaidi kulilo kununua
USHAURI MUHIMU
Iwe unaamua kununua au Kujenga nyumba yako hakikisha unajenga nyumba au KUNUNUA nyumba ambayo unaweza kumudu gharama zake na ni nyumba utakayoifurahia
Uwe unataka kujenga nyumba au kununua blchomes tutaweza kukusaidia kufikia malenho Yako
Blchomes tutakusaidia kujenga nyumba yako ya kisasa , kuchora ramani , kujua makadirio ya ujenzi (. BOQ ) na kufanya maboresho ya nyumba yako wasiliana nasi zaidi kupata ushauri bure , na NAMNA TUNAVYOWEZA kukamilisha ujenzi wa nyumba yako Wasiliana nasi zaidi whatsapp 0742892195
KAMA UNAHITAJI USHAURI ZAIDI KUHUSU UJENZI WASILIANA NASI ZAIDI 0742892195